Senegal, Umoja wa Ulaya, Marekani na Wadau wengine, jana walitia saini mkataba wa kufadhili utengenezaji wa chanjo nchini Senegal.
Hatua hiyo imechukuliwa katika wakati ambapo kuna upungufu wa chanjo na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona kutokana na wimbi la tatu la maambukizi lililokumba Bara la Afrika huku kukiwa na ukosefu wa Taasisi za kutengeneza chanjo Afrika.
Taarifa ya pamoja ya Serikali ya Senegal na Umoja wa Ulaya, imesema kuwa asilimia 95 ya chanjo zinazotumika Afrika zimeagizwa kutoka nje.
Taarifa hiyo imeongeza kwamba mkataba huo mpya wa ufadhili unanuia kuanzisha utengenezaji wa chanjo katika taasisi ya Pasteur mjini Dakar na kupunguza utegemeaji wa chanjo kutoka nje, Waziri wa masuala ya uchumi wa Senegal Amadou Hott amesema kuwa hatua hiyo itaweka msingi wa uhuru wa kimatibabu na dawa.
MTANZANIA ALIESHIRIKI MAZISHI YA TB JOSHUA, MKEWE, KABURI LAKE, UMATI MAZIKONI