Mkurugenzi wa Mipango wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Kulthum Mansoor (57) aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusota mahabusu kwa miaka miwili.
Hatua ya Kulthum kuachiwa kwa dhamana inakuja baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo akiomba kumbadilishia Kulthum ikiwemo ya utakatishaji fedha.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi (DPP) aliwasilisha ombi hilo kubadilisha hati ambapo alisomewa masharti ya dhamana na ametakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua na vitambulisho vya Taifa au vitambulisho vinavyotambulika watakaosaini bondi ya Sh.Mil. 20.