Marekani imetangaza kuipatia Tanzania zaidi ya dozi milioni 1 za chanjo dhidi ya COVID-19, msaada huo umetolewa kupitia mpango wa usambazaji chanjo wa COVAX kwa uratibu wa Umoja wa Afrika.
‘Marekani ina furaha kutangaza kuipatia Tanzania zaidi ya dozi milioni moja za chanjo dhidi ya COVID-19, msaada uliotolewa kupitia mpango wa usambazaji chanjo kimataifa wa #COVAX kwa uratibu wa Umoja wa Afrika’– Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania
‘Marekani inachangia chanjo hizi ili kuokoa maisha na kuiongoza dunia katika kulitokomeza janga hili. Aidha, kuchangia kwetu chanjo hizi ni kielelezo cha uimara wa ubia wetu wa miaka 60 na dhamira yetu ya dhati kwa Tanzania‘- Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania
‘Tutaendelea kuchangia chanjo salama na zenye ufanisi kwa wingi kadri itakavyowezekana, kwa watu wengi duniani kadri itakavyowezekana na kwa haraka kwa kadri itakavyowezekana hadi pale janga la COVID-19 litakapokuwa limetokomezwa kabisa’-Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania
CORONA TANZANIA: VIFO 29, WAGONJWA WAPYA 176 NDANI YA SIKU MOJA