Rais wa Tunisia Kais Saied amemfuta kazi Waziri Mkuu wa Nchi hiyo Hichem Mechichi na amesitisha pia shughuli zote za Bunge, kufuatia maandamano ya Wananchi jana Jumapili wakikilaumu Chama tawala kuwa kimeshindwa kutimiza matakwa ya Wananchi na kuongoza ipasavyo na pia kwamba hakijachukua hatua thabiti za kupambana na Corona.
Chama Tawala nchini humo kimemlaumu Rais na kusema alichokifanya ni sawasawa na kufanya Mapinduzi ya Serikali na kudai amekiuka katiba.
WAGONJWA WA CORONA WAFIKIA 682 TANZANIA, MISONGAMANO MARUFUKU NCHI NZIMA “BAADHI WANAFARIKI”