“Leo kwenye Daraja la Kijazi kama ukienda kuna Watu wanauza supu ya utumbo na miwa pale chini, jamani sio kila eneo ni la kupika au kufanya biashara, kwa sasa tumeanza kuandika mabango ya kuzuia Biashara baadhi ya maeneo”
“Mkakati wa sasa Dar es salaam kila Barabara inayojengwa lazima iwe na taa, sehemu yoyote yenye uhakika wa usalama Watu watafanya biashara saa zote, matukio yaliyokuwepo nyuma tumeyapunguza kwa asilimia kubwa”
“Vitambulisho vya Wajasiriamali vipo katika kuwawezesha Wajasiriamali, awamu hii Vitambulisho vinaboreshwa zaidi kuongezwa taarifa zingine muhimu ziwasaidie pia kupata mikopo na kuweza kuwafatilia wako wapi, nia kuwawezesha Wajasiriamali wafanikiwe zaidi “
“Mimi kama Mkuu wa Mkoa inatajwa moja ya majukumu yangu ni kusimamia hizi Halmashauri na fedha zinazopatikana zinadhibitiwa ili zitumike kwenye matumizi sahihi yaliyopangwa” ———Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla via Clouds360.