Ni Agosti 26, 2021 ambapo chama cha Soka Wanawake Tanzania na timu ya taifa ya Twiga Stars wamekutana na Vyombo vya Habari kuzungumza mengi yakiwemo kauli ya Rais kuhusu Chanjo kwa wachezaji pamoja na mengineyo.
Kauli ya Rais waandishi wa Habari baadhi ya Makundi mengine ya Watanzania wamechukulia kama jambo la siasa, msichukulie kauli kwenye negative way, Mama Samia sio Rais tu ni Mzazi kwetu, siku zote mzazi anapokuambia jambo ni la kukuonya na kukukanya ili utoke kwenye maadili ambayo anaona yeye sio mazuri uende kwenye maadili yanayompendezaa yeye na Jamii kwa ujumla”- Janeth Christopher, Mchezaji (Kiungo) wa Mpira wa Miguu wa Wanawake
“Hii kauli ya Rais Waandishi wa Habari wengi mnaichukulia katika siasa au haiendani na maadili ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ila sio kweli hii Mama kaitoa kama chachu kutuendeleza tuonekane kama Wanawake na sio kama Wanaume” “Sisi tumelipokea vizuri kama Rais ambaye anashikilia Nchi anasema neno kama hilo ameona kitu, sisi tunalichukulia vizuri, nawaomba msitugombanishe na Mama, mchukulie katika positive way”-Janeth Christopher, Mchezaji (Kiungo) wa Mpira wa Miguu wa Wanawake
“Kuhusu suala la kuvaa kiume wengi tupo kwenye mitandao ya kijamii tunaona au huko majumbani, mitaani sio Wachezaji wa Kike pekee ndio wanavaa pensi au jeans za kiume hata Watu ambao hawashiriki mpira wa miguu wa kiume wanavaa lakini kwakuwa tumeshajenga fikra kwamba haya mavazi Mtu akivaa ni Mchezaji kwahiyo hata ukimuona mwingine sio Mchezaji ila kavaa hivyo”-Janeth Christopher, Mchezaji (Kiungo) wa Mpira wa Miguu wa Wanawake
“Sio kila anayevaa hivyo ni Mchezaji hapana, mbona sisi tunavaa kikike na tunapenda!?, tunasuka, tunajipodoa, tunamake-up tunafanya vitu vingi, havitubudilishi sana kwenye kuwa Wanaume tunatakiwa kuwa Wanawake, muda mwingine Mtu anavaa kile anachoona kinampendeza” —Stumai Abdallah.
“Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu kwa utendaji wake na masuala mazima anayoendelea kuyafanya katika Soka la Wanawake, amekuwa akitu-support sana, amekuwa na sisi kama Mlezi na namshukuru kwa kudhamini CECAFA Women’s Championship itatuletea chachu katika Mpira wa Miguu wa Wanawake”-Janeth Christopher, Mchezaji (Kiungo) wa Mpira wa Miguu wa Wanawake
KAMA MOVIE:ASKARI ALIVYOPAMBANA NA MTU MMOJA ALIEKUWA AKIFYATUA RISASI OVYO DSM
“ANGEKUWA HAI TUNGEFAIDIKA NAE KWA MAMBO MENGI, POLISI WAMETUMIA BUSARA NA KAZI KUBWA”———RC DSM