Jinsi teknolojia inavyokua kuna baadhi ya vitu kwenye miaka inayokuja vitashindikana kufanyika kutokana na maboresho yanayofanyika kuvidhibiti.
Unaambiwa kuna simu ya mkononi iliibwa lakini baadae kidogo ikatuma ujumbe mfupi na picha ya mwizi wa simu hiyo kuonyesha kuwa ndiye mmiliki wake.
BBCSwahili.com wameandika polisi katika eneo la Essex nchini Uingereza wanamtafuta mwizi wa simu hiyo aina ya HTC ambayo iliibwa kutoka kwenye koti la mwanafunzi mmoja alipokuwa safarini kuelekea nyumbani.
Mwenye simu alikuwa ameweka kifaa cha usalama kwenye simu hiyo ambacho kinaifanya simu kumpiga picha mtu anapojaribu kuingiza namba ya siri au PIN mara tatu bila kufanikiwa.
Msemaji wa polisi alisema kuwa simu hiyo ilimpiga picha mwanaume huyu alipojaribu kuingiza namba hiyo bila kufanikiwa ambapo email ya Mwanafunzi huyo ndio ilituma ujumbe kwa polisi kuwataarifu kuhusu wizi huo.