Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa leo Bungeni Dodoma ameipongeza Club ya Simba kwa kuupiga mwingi na kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
“Nitumie fursa hii kuendelea kusisitiza umuhimu wa michezo kwa kuvipongeza vilabu vyetu vya mpira wa miguu vinavyoshiriki kwenye mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) na Ligi Kuu Zanzibar (PBZ Premier League), hakika kwa mpira mzuri wanaocheza wanakonga mioyo ya washabiki wa mchezo wa mpira wa miguu nchini”
“Kipekee niipongeze timu ya Simba Sports Club kwa kupeperusha bendera ya Taifa letu katika mashindano ya Shirikisho la Klabu Afrika, mwenye macho haambiwi tazama, sote tumeshuhudia wakiendelea kuupiga mwingi na kutuwakilisha vema katika medani za kimataifa” – Waziri Mkuu Majaliwa
“Niwapongeze pia wachezaji mahiri wa vilabu mbalimbali vya mpira wa miguu vikiwemo Yanga (Timu ya Wananchi); Simba (Wekundu wa Msimbazi) Namungo (Wauaji wa Kusini), Azam (Wazee wa Lambalamba) Biashara United (Wanajeshi wa Mpakani), Dodoma Jiji (Walima Zabibu), Tanzania Prison (Wajelajela) na bila kuwasahau Mtibwa Sugar (Wakata Miwa na Kagera Sugar / Wanankurukumbi) Vilevile, nivipongeze vilabu vya Zanzibar vikiwemo KMKM, Mlandege, Malindi, Mafunzo na vilabu vinginevyo” ——— Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
MBUNGE MUSUKUMA AIBUKA NA BUNGE LIVE ‘KUNA WABUNGE VILAZA, SIO KUONGEA KINGEREZA BILA SABABU