Baada ya miaka 12 Serikali ya Tanzania imesaini mkataba wa uzalishaji na ugawanaji mapato (PSA) kitalu cha RUVUMA – MTWARA.
Mkataba huu unaweka utaratibu wa serikali kupata zaidi. Kwa mara ya kwanza Serikali inapata kwenye Mapato ghafi (Gross) ambapo Kwenye huu mkataba serikali inapata 75%, ukilinganisha na huko nyuma ambapo ilikua inapata 68% kushuka chini.
Mara baada ya kusaini mkataba huo Waziri wa Nishati, January Makamba amesema >> “Siku hii ni kubwa na ya Kihistoria sababu Serikali inaenda kupata asilimia 75 ya Mapato Ghafi. Hii ndo tafsiri ya win-win na kazi hii imefanywa ndani ya mwaka mmoja. Wito wangu kwa wawekezaji ni SPIDI SPIDI SPIDI! Nawataka tufanye kwa haraka. Nataka ndani ya miezi 12 hadi 18 tuanze kutumia hii Gesi”. – Waziri Makamba.