Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Afisa Tawala Mwandamizi Flora Mgonja ameshiriki hafla ya Uzinduzi wa Pikipiki aina ya UM Motors iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika hafla hiyo ametoa wito kwa bodaboda huku akiwataka kuvitunza vyombo hivyo kwa kuzingatia sheria na usalama barabarani
“Kazi ya bodaboda ni ajira bodaboda ni maisha sisi kama serikali tunaunga mkono juhudi za Kampuni hii na wadau wengine wote fursa kama hii vijana tusiziacha tuwaunge wenzetu wa UM Motors vijana tuwe mabarozi wa kwenda kuwaeleza wenzetu kuhusiana na hii, vyombo hivi ni vizuri lakini tusipo vitumia vizuri pia ni hatari lazima tuvitumie ilikupata mafanikio tutumie kwa kuzingatia sheria na Usalama barabarani”–Afisa Tawala Mwandamizi Flora
Nae kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu TBS Dkt Athumani Yussuf Ngenya amesema kuwa vyombo hivi vya usafiri vinachagiza kwenye kuleta maendeleo ya Nchi
“Serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan nadhani mnaona wote jinsi gani inajitahidi katika kuhakikisha barabara zetu ziko salama na nzuri, hivi vyombo ni vizuri na vinaleta maendeleo lakini pia tukumbuke kwamba usalama ni muhimu sana na tukizingatia wiki hii ya nenda kwa usalama basi tuvitumie vyombo hivi vizuri tuhakikishe kwamba tunazingatia matumizi mazuri ya barabara, nichukue nafasi hii kuwapa hongera Kampuni ya UM Motors”-–Dkt Athumani Yussuf Ngenya