Wiki chache tangu kutoka kwa taaarifa za uhusiano wa kimapenzi kati ya Ney wa Mitego na Irene Uwoya ambazo Ney alizikataa, leo kuna nyingine ambazo pia zinamuhusu Irene Uwoya na msanii anaesemekana waliingia kwenye makubaliano ya kuwa mtu na meneja wake.
Msami ambae ni staa wa single ya ‘sound track’ amehusishwa na uhusiano wa kimapenzi na Irene Uwoya.
Haya ni majibu ya Msami alipoulizwa juu ya uhusiano na Irene Uwoya>>’Nipo na uwoya kivipi? hizi stori sijui nani kakupa bwana’
Majibu ya mpenzi wa Msami anaitwa Rehema>>’Maswali gani hayo mpigie mwenyewe muulize kifupi yeye ana mambo yake mwenyewe hamna lolote tamaa za vijana wanapotoka wanashawishika na tamaa ya hela, sijui wanajifanya wao meneja,yule mimi kuniacha ni ngumu sana yaani hata apite nani na nani kuniacha mimi hawezi yaani nina uhakika huo na najua mpaka jana nawasiliana nae yaani yule chapa ilale sisikii wivu’
‘Mimi najiamini na najikubali kwamba hata nikitokea hawezi kuongea chochote Msami, hata Uwoya simuogopi kwa sababu staa? maana hata mie staa, hawezi kuwa anammiliki maana kama angekua anammiliki asingekua na ruksa Msami akamwambia nina mwanamke wangu ana hivi na hivi maana hata uwoya mwenyewe ananijua’
‘Yeye mwenyewe anatakiwa kujiheshimu kwanza ajitazame yeye mkubwa halafu lazima ajihesabie katembea na watu wangapi na nasikia taarifa yake kuwa yeye kawaida yake yaani kila mtu mtaani analalamika, anajishusha sana tofauti na wenzake wanaojiheshimu, kwa sababu sio rika lake kwa mtu anayejiheshimu hawezi kufanya hivyo’.
picha: www.makorokocho.co
87.8 Clouds Fm inasikika ukiwa Mbeya.
Bonyeza play kusikiliza hii You heard ya leo hapa chini
Ili niwe nakutumia kila taarifa inayonifikia jiunge na mimi kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.