Kutoka Kenya naambiwa ndani ya siku zisizozidi 32 watumiaji wa daladala maarufu kama matatu jijini Nairobi hawatoweza kutumia huduma hiyo endapo hawatokuwa na kadi maalum ya kulipia nauli ukiwa ni mfumo mpya wa ulipaji nauli tofauti na ule uliozoeleka wa kulipa cash mkononi.
Taarifa hiyo ya halmashauri ya uchukuzi nchini Kenya NTSA imetoa nafasi ya kutumia pesa taslimu kulipia nauli hadi July 1 2014 na baadaye mfumo wa digital utaanza kutumika [kadi kama za Atm zinazoitwa 1963 CARD] zitatumika kulipia nauli.
Sasa unaambiwa ili kumiliki kadi hiyo utahitaji kumpa konda wa matatu namba yako ya kitambulisho na namba za simu kisha utaweka pesa kwenye kadi hiyo kupitia huduma za kutuma pesa kwa simu.
Nauli itatozwa wakati kadi inapopitishwa kwa mitambo maalum ya kuchanja kadi ambapo kadi moja inaweza kutumiwa na watu wawili japo Makonda wengi wamependekeza kila mmoja awe na kadi yake.
Kwa sasa wamiliki mbalimbali wa matatu hayo wako kwenye hatua za kufanya majaribio na wanatarajia ifikapo Julai 1 2014 wataweza kuendelea na usafiri wao kama kawaida.
Kupitia mpango huu wa Dijitali-1963 CARD wamiliki wa daladala au matatu watapata pesa zao zote zinazokusanywa na konda ambao hawatokua wakibeba pesa taslimu na hivyo kuziba mianya ya pesa kutumika kwa kutoa rushwa kwa polisi pia.
Huu ni mpango ambao unatarajiwa kufikia katika miji mingine ya Kenya kwa awamu kote katika nchi ya Kenya ambapo aina hii ya ulipaji wa nauli itatumika kwenye jiji la Dar es salaam pia kwenye mabasi yaendayo haraka ambayo yako mbioni kuanza kufanya kazi.
Ili niwe nakutumia kila taarifa inayonifikia jiunge na mimi kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.