Huenda hujapata nafasi kufuaatilia kikao cha Bunge leo kinachoendelea Dodoma, moja kati ya mambo ambayo yamejadiliwa ni kitendo cha baadhi ya madaktari kusababisha matatizo makubwa zaidi kwa wagonjwa pamoja na vifo vinavyotokana na uzembe, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii ametolea majibu suala hilo.
“.. Iwapo mgonjwa amefika katika hospitali ya Serikali.. akaangaliwa na kutibiwa na daktari na kuandikiwa dawa zinazohusiana na maradhi aliyokuwa nayo.. na kwa bahati mbaya dawa hizo ikawa hazipo na hazikupatikana kwa mgonjwa huyo.. Na mgonjwa huyo akapoteza maisha.. je wanafamilia wa mgonjwa huyo, wanayo haki ya kuishtaki Serikali kutokana na kifo cha mgonjwa aliyekosa dawa..” – Haroub Mohamed Shamis, Mbunge wa Chonga, Zanzibar.
Akijibu swali hilo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashidi amesema;- “..Mazingira ya utoaji huduma za afya duniani kote zinaenda sambaba na uwezo wa kituo, taaluma waliyokuwa nayo, na mazingira waliyokuwa nayo wakati wakiwa wanatoa huduma zile.. na kwa hiyo watahukumiwa kwa kiwango walichokuwa nacho na kushindwa kutoa huduma kwa kiwango kile walichokuwa nacho wakati ule.. Mgonjwa huyo hakunyimwa dawa wakati dawa ikiwepo kwenye kituo.. maana yake kama dawa hizo hazipo kwenye kituo, huyo mgonjwa hajanyimwa dawa.. Hakutakuwa na kosa la kuishtaki Serikali, au kushtaki kituo, au kumshtaki huyo daktari kwa kushindwa kutoa dawa ambayo haikuwepo kwenye kituo..”
Kusikiliza sehemu ya taarifa hiyo bonyeza play hapa.
Unaweza kuweka comment yako hapa mtu wangu kuhusiana na habari hii.