Ni siku moja imebaki ili tuzishuhudie sherehe kubwa za utoaji wa tuzo za CHOAMVA Afrika Kusini, mshiriki pekee wa Tanzania Diamond Platnumz kupitia muziki wake kuna vingi ambavyo vinaendelea kutokea na amekuwa mjumbe wa kuiwakilisha Tanzania katika ishu mbalimbali kupitia muziki huohuo anaoufanya.
Jana Novemba 27 alikuwa ndani ya Jumba la BBA Afrika Kusini na mwanamuziki Fally Ipupa wakiwa na ujumbe wa ONE Campaign kuhimiza kilimo, leo taarifa ninayokupa ni kuwa amekuwa mmoja ya wasanii ambao wamewakilisha nchi zao za Afrika katika kuuwasilisha ujumbe ambao unahimiza mapambano dhidi ya Ebola, ambapo wasanii wengine ni pamoja na Akon (Senegal), Fally Ipupa (DRC), Angélique Kidjo (Benin), Danai Gurira (Zimbabwe) Ice Prince, Femi Kuti, Desmond Elliot na Praiz (Nigeria); Mafikizolo na T-bo Touch (South Africa), Victoria Kimani (Kenya), Diamond Platnumz (Tanzania) na Magasco (Cameroon).
Wanamuziki hao wamewasilisha ujumbe wa kuwataka viongozi kote Duniani kufanya jitihada za kupambana na Ebola, pamoja na kuwahimiza watu kusaini maombi maalum yaliyopo katika mtandao wa ONE Campaign (www.one.org/) ambao unawahimiza viongozi Duniani kupambana na Ebola.
Diamond na Waje ni wasanii pekee walioiwakilisha Afrika Mashariki kwenye Kampeni hiyo ya kimataifa ambapo wasanii wote wamewasilisha ujumbe wao kwa mabango yenye ujumbe maalum na hakuna sauti ya msanii yoyote iliyosikika.
Hii ni video ya Kampeni hiyo ambayo imepewa jina la “Ebola: What are we waiting for?”
Ni ahadi yangu kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook