Huenda umepokea simu, sms, au umesoma story zilizoenea kwenye mitandao kuhusu taarifa za kikundi cha wezi wanaojiita Panya Road kuvamia maeneo mbalimbali na kupora vitu, ikiwemo maeneo ya Sinza na Mwananyamala, pamoja na kujeruhi watu.
millardayo.com inaendelea kufuatilia kuhusu tukio hilo, ikiwemo kumtafuta Kamanda wa Polisi Dar, nitakufahamisha kinachoendelea kuhusu tukio hilo.
Hizi ni baadhi ya tweets zilizonifikishia taarifa hiyo.
Niko kwenye #AMPLIFAYA sasa hivi na nasikia taarifa nyingi za kundi la Wezi (Panya road) Kinondoni na Sinza, kama una taarifa zao naomba
— millardayo.com (@millardayo) January 2, 2015
@millardayo Msaada wa jeshi la polisi unahitajika haraka maeneo ya manyanya kinondoni,kuna vijana wanavunja na kupora maduka,wako wengi!
— Shilinde! (@Erickshilinde) January 2, 2015
Nimeongea na @Izzo_bizness anasema Panya Road walianza kuingia mtaani kwao leo ila jirani akapiga risasi kama tatu juu wakatawanyika.
— millardayo.com (@millardayo) January 2, 2015
Suzy anaripoti hali sio nzuri wale Panya Road (kundi la wezi) wanapita nyumba hadi nyumba, maduka na kwenye magari wanaiba kwa nguvu — millardayo.com (@millardayo) January 2, 2015
@millardayo panya rodi jamani wameingia mwenge ukuuu — aristides kessy (@Aristides_Kessy) January 2, 2015
Mtangazaji Kibonde ni miongoni mwa waliovamiwa na kundi la Panya Road Dar leo, walilala chini kwenye Baa, wengine wameumizwa kwa kupigwa — millardayo.com (@millardayo) January 2, 2015