Maswali yamekua mengi watu wakijiuliza kuwa hii Mkata mkaa ni kundi jipya? na kama ni kundi linaundwa na watu wangapi? na vipi kuhusu Tip Top na Tmk Wanaume Family?
Temba kutoka Tmk Wanaume family ameongea na millardayo.com na kutoa ufafanuzi juu ya hilo jina kwa kusema >>’Wakata mkaa tunabaki palepale ni watu wanaofanya kazi ngumu, ni jina jipya tulilokuja nalo lakini ni walewale Tmk Wanaume Family ila tumewaongeza watu wengine ambao ni rafiki zetu kama Madee na Julio ingawa utawasikia watu wengine wakiwemo Watangazaji pia wakiwa wanawakilisha Wakata Mkaa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook