Kifungo cha nje alichohukumiwa staa Chris Brown kutokana na kosa la kumpiga Rihanna, miaka sita imepita lakini hukumu hiyo bado inaendelea kumgharimu staa huyu.
Iliandaliwa ziara yake ya muziki yenye jina la ‘Between The Sheets’ iliyokuwa ianze kufanyika leo, imebidi kuahirishwa kutokana na Chris kutakiwa kumalizia saa 100 ambazo zimebaki kwenye adhabu aliyopewa ya kufanya kazi za kijamii kwa saa 1000.
Hakimu anayesimamia kesi hiyo aligoma kumpa ruhusa Chris ili akafanye tour hiyo kisha arudi kumalizia adhabu yake.
Chris ameandika kwamba anafanya juhudi za kuimaliza adhabu hiyo ili awe huru na kazi zake.
Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram staa huyo aliomba radhi kwa usumbufu kwa mashabiki wake na kusema show haijafutwa bali imesogezwa mbele, itafanyika tarehe ambayo bado haijatajwa.
“I would first like to apologize to all the fans and people who have been supporters of me and all the music over the years. The beginning of the BTS tour has been moved to later dates now. The judge would not sign off on my travel to do the tour until I finish these last 100 hours of community service. I promise that I am busting my ass doing it everyday until it’s complete. This is the most disappointing news I’ve gotten in a while. Everything happens for a reason so I wanted to personally inform my fans. The show must go on. Out of 1000 hours I only have 100 left. I will work my ass off to complete it and I will be on that stage. Once again I’m sorry for the delay. I love yall! We will let yall know the dates that are changed. It’s not cancelled. Just moved around a couple weeks.”– @chrisbrownofficial
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter, instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook