Kikao cha Bunge kimeendelea leo Dodoma, wakati wa maswali na majibu moja ya ishu ambayo iliulizwa ni kuhusu Serikali inafanya jitihada gani kuzuia movie ambazo ziko kinyume na maadili ya Tanzania.
“Serikali imeshafanya tafiti zozote zile zinazoonyesha athari ni kwa kiasi gani utamaduni wetu umeathirika? kwa kuwa kasi ya utandawazi ni kubwa sana sana na kasi ya Serikali kuwisha au kuimarisha hizo sera na sheria ni ndogo sana na kundi linaloathirika ni vijana, Serikali haioni kasi hiyo ndogo waliyonayo itaangamiza nguvu kazi ya Taifa na kupoteza tamaduni zetu zote?”– Mbunge Amina Mwidau.
Akijibu kuhusu suala hilo Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia amesema; “Serikali kwa upande wake tuna vyombo mbalimbali vinavyosimamia jambo hili, kwanza ni bodi ya filamu ambayo husimamia filamu zinazotoka nje na ndani ya nchi ili kuhakikisha zinazoingia kwenye soko zinafuata maadili, tuna Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA kazi yake ni kuhakikisha lugha iko sawa, lakini pia tuna kamati ya maudhui ipo chini ya TCRA kazi yake ni kusimamia maudhui“
Baada ya majibu hayo Mbunge Maryam Msabaha aliuliza; “Wasanii wengi wanaiga mambo ya kimagharibi na filamu zao nyingi wanazozionyesha zinakiuka maadili ya Mtanzania, Je Serikali inachukua hatua gani kuzuia filamu hizo?”
“Hakuna filamu inayoingia sokoni bila kutazamwa na kuruhusiwa na bodi ya filamu na inahakikisha haiharibu utamaduni wa mtanzania, tunajua zipo zinazoingia kwa njia ya panya lakini kuna njia ambazo tunatumia kuwakamata, zipo filamu nyingine zimeteketezwa kutokana na kutoridhika nazo“– Juma Nkamia.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook