Baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kutangaza kusogeza mbele zoezi la uandikishwaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wamezungumzia juu uya suala hilo.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Libuva alitangaza hatua hiyo wakati wa mkutano wa pamoja baina ya viongozi wa vyama vya siasa na NEC kujadili zoezi la uandikishwaji wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura chini ya mfumo mpya wa electronic (BVR).
“Kwa kweli tuna matatizo makubwa kwa sababu pamoja na kukutana na tume ya uchaguzi ya taifa na kuelezwa kwamba sasa uchaguzi wa kujiandikisha utaanza tar 23 katika mkoa wa Njombe hatukupata fursa wala hatukupewa ratiba kamili ya uandikishwaji wa wapiga kura katika maeneo yote vile vile hatukupewa ratiba kamili ya vituo vya kuandikishia wapiga kura hapa Njombe na mikoa mingine” Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba
“Ni kweli NEC imesogeza mbele uchaguzi haujafanyika… mimi naona ni sahihi kwa sababu najua huu mfumo haujaeleweka … nashukuru kama tumekukubali kuongeza wiki moja ili tuendelee kujielimisha kuhusu mfumo na kuona namna gani tutashiriki kikamilifu bila kuja kupata matatizo mbele ya safari“– Augustine Mrema, Mwenyekiti wa TLP.
“Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ni hatua ya msingi sana katika kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao lakini hata kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa inakuwa huru inakuwa haki na inashirikisha watu wengi.. mchakato wa kuliboresha daftari hili usipoenda vizuri unaweza ukasababisha nchi yetu ikachafuka na tunayo mifano mingi katika nchi nyingine. Uamuzi wa kusongeza mbele kwa lengo la kuboresha mchakato mzima ni umauzi wa busara… tujihakikishie kwamba zoezi litakwenda vizuri kila anayetakiwa kushiriki ataridhika” Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM.
Bonyeza play kusikiliza mazungumzo hayo kutoka kwenye Show ya Power Breakfast.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook