Habari za Mastaa

Drake na ‘Suprise’ yake ya album kama Beyonce!

on

theMkali wa tuzo za Grammy Drake ameamua kuiga style ya Beyonce ya bila kutangaza kutoa albamu kwa kuachia albamu yake mpya yenye nyimbo 17 kwa kuwashtukiza mashabiki wake.

Drake alitoa albamu yake hiyo inayoitwa ‘If You’re Reading This It’s Too Late’ jana Alhamisi kwa kuipost kwenye Twitter ambayo amewashirikisha mastaa mbalimbali kama Lily Wyne, Travi$ Scott na PartyNextDoor,

Drake ameendelea kufanya vizuri ambapo katika albamu yake iliyopita ya ‘Nothing Was the Same’ aliweza kufanya vizuri na kushika nafasi ya kwanza katika billboard mwaka 2013 na kufanikiwa kuuza kopi 658,000 katika wiki ya kwanza tu.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter,  Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments