Inawezekana ukawa na hamu ya kufahamu ni idadi ngapi ya movie zinazopitishwa ambazo zimefanyiwa marekebisho na kufaa kimadili, sasa leo nakukutanisha na Bodi ya Tanzania ambao huwa wanahusika kuzipokea filamu zote za Tanzania na kuzipitisha.
Akizungumza kwenye AMPLIFAYA ya Clouds FM, Bi. Joyce Fisso Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania alisema;..”kati ya filamu 447 , filamu 47 zilihitaji marekebisho na tunaposema marekebisho kwamba ni kuna vipengele ambavyo tunaona vinaweza kurekebishika na visiharibu hadithi lakini vile vile visikizane na sheria yetu na bahati nzuri wadau wetu wote wamerekebisha na kurejesha
Millardayo:..’Sasa hivi kwa Tanzania mnapokea filamu ngapi kwa mwezi?…”
Bi.Joyce:..’Kwa mwezi tunapokea kati ya filamu 40 mpaka 100, lakini kati ya Julai mpaka mwaka huu sasa tumeshapokea filamu 447 kwa maana ya majina lakini kama unavyojua filamu zetu nyingi ni part 1 na part 2 kwa hiyo kati hizo za part 1 na part 2 ni zaidi ya 660..“
Unaweza uka bonyeza play kusikiliza interview hapa