Hekaheka ya leo inahusu tukio la mama mmoja maeneo ya Tabata, Dar es salaam kupigwa risasi na vijana wawili wakati akitaka kulipia fremu ya duka maeneo ya karibu na nyumbani kwake.
Anasema wiki iliyopita baada ya kukubaliana na wahusika wa fremu hiyo kwenda kulipia kuna vijana wawili walimfuata na kumtaka awape pochi ambayo ndani kulikuwa na pesa za kulipia fremu pamoja na pesa zake nyingine.
Anasema alikubaliana na msichana aitwaye Anna ili kwenda kulipia fremu hiyo na alipofika baada ya mazungumzo…yule msichana akaenda kuchukua funguo ili kuangalia ndani ya fremu hiyo.
Anasema baada ya dakika3 wakaja vijana wawili wakamnyooshea bastola…wakazozana kwa muda mrefu kisha wakamnyang’anya pochi yake..kabla hawajaondoka wakampiga risasi ya kifuani.
Anasema kilichomshangaza yule msichana aliyemsisitiza aje na pesa hakumuona tena baada ya tukio hilo…na alipiga kelele za kuomba msaada lakini hakuna mtu aliyemsaidia..baada ya kuona hivyo akawasha gari lake na kwenda nyumbani..alipofika majirani wakampeleka Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Msikilize hapa mwenyewe akimwelezea Geah Habib…
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE