Adele ndiye staa wa muziki anayefunga mwaka wa 2015 kwenye headlines za burudani Marekani na dunia nzima akiwa ameuza zaidi ya nakala milion 5 za single yake mpya ‘Hello’ huku video yake ikiwa imegusa watazamaji milion 700 kwenye mtandao wa YouTUBE! Ujio mpya wa Adele kwenye kurasa za burudani umepokelewa kwa muamko mkubwa sana duniani.
Nimekutana na interview ya Adele na jarida la TIME Magazine la Marekani na ndani yake staa huyo amegusia vitu vingi ikiwemo album yake mpya 25, social media pamoja na mauzo ya juu nchini Marekani.
Hivi ni baadhi ya vitu alivyovigusia Adele na interview yake na TIME Magazine:
Mauzo ya nakala zaidi ya mamilioni Marekani: “Inashangaza kidogo na kunishitua sana. Ukizingatia mimi hata sio Mmarekani. Labda wanafikiri nina undugu na Malkia…“
Mtazamo wake kuhusu kuitwa ‘Brand’: “Kila mtu analitumia neno hilo. Sipendi kuitwa ‘brand’ wananifanya nionekane kama aina fulani ya bidhaa au kama packet la kripsi… msanii ni package ya vitu vingi!“
Kwanini watu huupokea vizuri muziki wake: “Uhalisia nilionao ni kwamba sioni aibu kuimba ukweli unaonigusa hata kama mimi ndio mwenye makosa. Kila mtu hufanya makosa. Watu wengi hujifanya wajasiri kwasababu wanaogopa kuonyesha udhaifu wao. Mimi najaribu kuimba nyimbo zinazogusa vitu vya ukweli kwa mashabiki wangu kwa sababu kama mimi hata wao wanaumizwa na vitu mbalimali maishani japo natumaini pia nyimbo zangu zitaleta furaha kwenye maisha ya mashabiki wangu na sio huzuni na machungu“.
Mitandao ya kijamii ina nafasi gani kwake: “Napenda kuweka mambo yangu private… kuwa na privacy inakuwezesha kuandika nyimbo za ukweli utakaogusa watu, waupende au wasiupende bado utakuwa ukweli. Maisha yangu yamebadilika sana toka niachie ‘Hello’ na hiyo inanipa changamoto, hivyo siwezi kukaa kusubiria likes milioni na kwa picha moja… nitapata wapi muda wa kutunga nyimbo zitakazogusa watu? Huo sio uhalisia“.
Maisha yake binafsi ya nyumbani yapoje: “Nina maisha ya kawaida, nahisi watu wengi wangekuwa wanajua jinsi ambavyo maisha yangu ni ya kawaida wangeshangaa. Kama sina kazi zozote huwa nashinda tu nyumbani na familia yangu… ni muhimu kutokupagawa na hivi vitu, ni muhimu pia kukumbuka kuishi kama watu wengine wote wa kawaida“.
Kuhusu kufanya Collabo na wasanii wengine?: “Album yangu 25 haina collabo yoyote lakini hiyo haimanishi hakutakuwa na collabo kwenye album yangu ijayo baada ya hii… zile tetesi za mimi kukataa kushirikiana na Beyonce hazikuwa za ukweli, sikuweza kufanya collabo na mtu kwenye album hii kwa sababu nilikuwa nashindwa kugawa muda na kufanya maamuzi ya kufanya kazi na nani...”
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.