Kati ya wasanii ambao mwaka huu umetokea kuwa poa sana kwao huwezi kuacha kulitaja jina la staa wa muziki kutoka Uingereza, Adele… Hivi karibuni Adele aliziteka headlines na ujio wa single mpya ‘Hello’ single inayopatikana kwenye album yake mpya iitwayo 25.
Nimetembelea mtandao wa YouTUBE na huko nimekutana na interview aliyoifanya Adele siku chache zilizopita, ndani yake aligusia vitu vingi lakini vikubwa alivyoviongelea zaidi vinahusiana sana na ujio wake mpya kwenye chati za burudani, single yake mpya na nguvu ya mitandao ya kijamii.
Haya ni machache niliyoweza kunasa kupitia interview hiyo:
Mtazamo wake kuhusu social media: “Nilikuwa sijui jinsi gani ambavyo mitandao ya kijamii ina nguvu… mara ya kwanza nilitaka kuachia wimbo wangu kwa njia ya kawaida lakini ikashindikana baada ya management yangu kuniambia kuwa siwezi kuwa ‘old school’ kwenye dunia ambayo mitandao ya kijamii inaendesha karibia kila kitu… badaaye baada ya zile tweets 2 za mwanzo za ‘Hello’, website yangu ikaanza kupata watazamaji 4,000 kwa sekunde. Sikuamini! Yote ni kutokana na nguvu ya mitandao ya kijamii.“
‘Hello’ inamhusu nani maishani mwako?: “Hello inamhusu kila mtu, ni single ambayo nilitaka iwakumbushe watu kuwa bado nipo licha ya mambo yote yaliyotokea [na kunitokea mimi], na ninawafikiria kila siku iendayo kwa Mungu… Pia ni single moja romantic ya kimapenzi ambayo inaweza ikamgusa mtu yoyote yule muhimu maishani mwako.“
Kwanini uliamua kuachia single ya ‘Hello’ kama single yako ya kwanza?: “Nafikiri baada ya kupotea kwa muda kidogo kwenye game nilihisi [nakuamini pia] kuwa neno ‘hello’ lilikuwa neno zuri zaidi kwa mimi kutumia ili kurudi kwenye muziki. ‘Hello’ pia inasaidia kutambulisha album yangu sokoni [inakuwa rahisi kwa watu kutaka kununua album yangu kwa sasa] pia ni neno la ukarimu na lenye upendo kwa watu.“
Unachukuliaje umaarufu: “Sipendi umaarufu. Album yangu ya pili, ’21’ ilivyotoka mafanikio yakaanza kuja kwa kasi sana na album ikawa inazidi kufanya vizuri… niliogopa sana kwa sababu nilikuwa sielewi inakuwaje album inazidi kukua na kufanya vizuri na nimeshapokea tuzo nyingi. Media ikaanza kunipa attention kubwa sana na nikaanza kupotea kidogo kidogo na hicho ndicho kilichonifanya nijitenge na maisha ya camera na media na nilijiuliza ‘nitawezaje kutengeneza wimbo utakaowagusa watu wakati binafsi nipo bussy na vitu ambavyo havina uhalisia na maisha ya kawaida..“
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.