April 18, 2017 kupitia kipindi cha Sizi Kitaa kinachoruka kupitia Clouds TV rapa Lord Eyes amezumgumzia kuhusu kuwa kwake kimya kwa mda mrefu alisema amejifunza mengi katika kipindi hicho tangu Nako 2 Nako hadi WEUSI.
Eyes amedai kupata experience ya muziki kwa kuufatilia ndani ya miaka 17 akisema wananchi hawawezi kukuelewa kama utakuwa haujachia wimbo kwa sababu unawasiliana nao kwa kutumia wimbo akidai pia kutamani kuacha kufanya muziki.
>>>”Nilichojifunza, kwanza nimepata experience kubwa kwenye muziki. Nina zaidi ya miaka 15 ndani ya muziki. Wananchi hawakuelewi kama hauna wimbo hewani maana unawasiliana nao kwa nyimbo. So, unapoachia wimbo ndio unawasiliana nao.
>>>”Kuna wakati nilipokuwa nimekaa kimya nilitamani kuuweka kando na kufanya vitu vingine, lakini wananchi walinifanya nishindwe kuacha muziki maana wanangu walikuwa wanauliza mbona sitoi wimbo, mbona kimya? Hiyo ilikuwa kila mahali ninapokwenda. Kwa hiyo sasa hivi nimerudi, nimeona niwape dawa zao.” – Lord Eyes.
Alipoulizwa kuhusu kama kuna kitu anamiss kwenye Hip Hop, Lord Eyes alisema: >>>”Namiss real hip hop. Yaani namiss maisha halisi ya vijana wa mtaani na namiss muziki mzuri ambao ni hip hop. Unajua miaka ya 1990 kipindi ndio tunakwenda Secondary, watu walikuwa wanapenda hip hop na walikuwa wanaishi hip hop. Ndio kitu kilichonirudisha kwenye game na kunipush nikafanya Album. Sasa hivi nitaitoa mwaka huu na wimbo wa kwanza ndio huu nilioutoa. Hivyo wategeme muziki mzuri nitawarudisha miaka ya 1990.” – Lord Eyes
VIDEO: Staa wa Bongofleva Belle 9 amefiwa na baba yake