Kwenye headlines za burudani weekend iliyopita zilikuwa ni tuzo za muziki za All African Music Awards 2015 maarufu kama AFRIMA Awards zilizokuwa zinatolewa usiku wa jumapili (November 15) Lagos, Nigeria ambapo kutoka Bongo Flevani, Tanzania iliwakilishwa na watu wetu Diamond Platnumz na Vanessa Mdee.
Good news kwako mtu wangu, Tanzania kwa mara nyingine tena imeweza kujinyakulia tuzo 4, tatu zikibebwa na Diamond Platnumz na moja ikibebwa na hit maker wa single ya Hawajui na Nobody but Me, Vanessa Mdee!
Diamond Platnumz alikuwa anawania vipengele vitatu mwaka huu kwenye tuzo za AFRIMA Awards 2015 ambavyo vyote aliibuka mshindi, ‘Artist of the year’ kilichokuwa kinawaniwa pia na Alikiba, Davido, Wizkid, Yemi Alade, Jose Chameleone, Flavour na Sarkodie, ‘Best Male Artist in East Africa’ pamoja na ‘Song of The Year’ ambapo wimbo wa ‘Nasema Nawe’ uliibuka kuwa wimbo bora wa mwaka.
Mara baada ya kushinda tuzo yake ya kwanza ya AFRIMA, Diamond alipost picha kwenye page yake ya Instagram na ujumbe kwa mashabiki uliyosema…
>>> “ Just wanted to let you know that we have won the first one BEST EAST AFRICAN ARTIST OF THE YEAR! this isnfor you my fans… thanks for the Votes!!! thanks alot @the_speshoz for this Suit and many thanks to my brother @jm_international_collection for the scarf and Tie! #AfrimaAwards” <<<< @diamondplatnumz.
Baadaye ikawa zamu ya mtu wetu Vanessa Mdee kuweka headlines zake kwenye usiku wa tuzo za AFRIMA Awards 2015 baada ya kuibuka mshindi kwenye kipengele cha ‘Best African Pop’ kupitia hit single yake ya mwaka 2014 Hawajui, na mara baada ya kupokea tuzo yake Vee Money akashare na watu wake kwenye Instagram furaha yake kwa kupost picha na ujumbe uliosema….
>>>“ GLORY TO GOD IN THE HIGHEST”BestAfricanPop #Hawajuhi thankyou @Nahreel @barnabaclassic and #Tanzania #Africa for letting me sing my song this one is for you“<<< @vanessamdee.
Hizi ni baadhi ya picha za wasanii waliokuwepo na wasanii walioshinda tuzo kwenye usiku wa AFRIMA Awards 2015:
Na hapa ni orodha kamili ya washindi wote wa tuzo za AFRIMA Awards 2015:
ARTIST OF THE YEAR
Diamond Platnumz
SONG OF THE YEAR
Diamond Platnumz – “Nasema Nawe”, featuring Khadijo Kopa
ALBUM OF THE YEAR
Charlotte Dipanda – “Elle n’a pas vu”
BEST ARTISTE IN AFRICA (RnB & Soul)
Praiz Adejo – Nigeria
BEST AFRICAN REGGAE, RAGGA & DANCEHALL
Stonebwoy – Ghana
BEST MALE ARTISTE: INSPIRATIONAL CATEGORY
Darey – Nigeria
BEST FEMALE ARTISTE: INSPIRATIONAL CATEGORY
Betty Akna- Equatorial Guinea
VIDEO OF THE YEAR
Wiyaala – Ghana
BEST ARTISTE IN AFRICAN POP
Vanessa Mdee – Tanzania
BEST ARTISTE IN AFRICAN HIP HOP
Casper Nyovest – South Africa
BEST ARTISTE IN AFRICAN ELECTRO
Flavour – Nigeria
PRODUCER OF THE YEAR
Sauti Sol and Cedric Kadenyi – Kenya
SONGWRITER OF THE YEAR IN AFRICA
Joseph Chameleone – Uganda
REVELATION OF THE YEAR IN AFRICA
Adekunle Gold – Nigeria
MOST PROMISING ARTISTE IN AFRICA
Kiss Daniel – Nigeria
BEST ARTISTE IN AFRICAN CONTEMPORARY
Charlotte Dipanda
BEST ARTISTE IN AFRICAN JAZZ
Kunle Ayo – Nigeria
BEST MALE ARTISTE IN WESTERN AFRICA
Olamide – Nigeria
BEST FEMALE ARTISTE IN WESTERN AFRICA
Yemi Alade – Nigeria
BEST ARTISTE IN AFRICAN ROCK
M’vula – Kenya
BEST AFRICAN GROUP
Sauti Sol- Kenya
BEST AFRICAN COLLABORATION
AKA(South Africa) and Burna Boy(Nigeria)
BEST FEMALE ARTISTE IN SOUTHERN AFRICA
Busiswa Ngoku- South Africa
BEST MALE ARTISTE IN SOUTHERN AFRICA
Casper Nyovest- South Africa
BEST FEMALE ARTISTE IN NORTHERN AFRICA
Manal- Morocco
BEST MALE ARTISTE IN NORTHERN AFRICA
Ahmed Soultan- Morocco
BEST FEMALE ARTISTE IN EASTERN AFRICA
Tsedenia Gebremarkos- Ethiopia
BEST MALE ARTISTE IN EASTERN AFRICA
Diamond Platnumz- Tanzania
PILLAR OF CULTURE IN AFRICA
Bola Ahmed Tinubu (Jagaban)
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE