Watu wengi wamekuwa wapenzi wa magari mapya jambo ambalo huwafanya kufuatilia kwa karibu kila wanaposikia kuna aina mpya ya gari imeingia sokoni, lakini magari mapya yanadaiawa kuwa na athari mbaya kwa afya.
Kwa mujibu wa utafiti ni kwamba wamiliki wa magari wako hatarini sana baada ya kubainika kuwa huvuta hewa yenye viambata 10 million vya sumu katika kila pigo moja la kupumua wakiwa garini huku ndani ya magari mapya pekee kukiwa na viambata vya sumu mara 10 zaidi ya magari ya zamani.
Mmoja wa waliofanya jaribio hilo Nick Molden kutoka Emissions Analytics alisema: “Madereva na abiria wao wanaweza kuathirika sana kama wapo garini. Viambata hivyo ni vidogo sana – ambavyo sio rahisi kuonekana, lakini kukaa kwake muda mrefu ni mbaya kwa afya ya madereva.”
Jaribio lilifanywa kwa kuhesabu viambata vilivyochafuliwa kwa cubic centimetre ya hewa kwenye magari kwa zaidi ya saa nne katika uendeshaji wa mjini na kijijini ambapo ilibainika kuwa, hewa ya kawaida ina vijidudu, chavua na vumbi, lakini kiwango kidogo ni hatari kwa afya ukilinganisha na masizi yatokayo kwenye engine – hasa diesel.
Prashant Kumar, Professor wa Uhandisi wa Kimazingira katika Chuo Kikuu cha Surrey alisema: “Kama utasimama kwenye taa za barabarani ukiwa umejifungia vioo, sumu hii inakuwa kwa kiwango kikubwa.”
VIDEO: “Tutapokea taarifa na tutakuhifadhi, hatukusemi” – Waziri Mkuu Majaliwa. Bonyeza play kutazama.