Habari za Mastaa

Jay Z avunja rekodi katika chart za Billboard

on

Kwa mujibu wa mtandao wa Hypebeast umeripoti kuwa Rapper Jay Z amevunja rekodi  kwenye chart za Billboard Hot 100 wiki hii baada ya kuingiza jumla ya ngoma 100 kama solo Artist kwenye chart hizo  na kuwa msanii wa 6 kwenye historia.

Imeelezwa kuwa rekodi hiyo imekuja kupitia ngoma ya “Mood 4 Eva” aliyoshirikishwa na mkewe Beyonce na Childish Gambino ikiwa ngoma hiyo ipo kwenye album ya ‘The Lion King: The Gift’. Wimbo huo umeshika nafasi ya 90 kwenye chart za Billboard Hot 100 na kuufanya kuwa wimbo wa 100 wa Rapper Jay Z kuwahi kwenye chart hizo.

Jay Z ambaye ameshika nafasi ya sita kwenye list hiyo anaungana na wakali kama The Glee (207), Rapper Drake (196), Rapper Lil Wayne (163), Elvis Presley (109) na Rapper Nicki Minaj (103)

VIDEO: STAA ALIEACHWA NA BWANA KISA BONGO MOVIE  “PICHA ZILIVUJA, SIAMINI KATIKA KIKI”

Soma na hizi

Tupia Comments