Baada ya ndege mpya mbili za Air Tanzania zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuwasili nchini Leo September 28 2016 umefanyika uzinduzi wa Ndege hizo aina ya Bombadier Q400 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere Dar es salaam na mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli. Rais Magufli alipopata nafasi ya kuhutubia alizungumza mambo haya
'Ukitumia ndege za Jet kwenda Songea mafuta ni mil 28.9, lakini ndege hizi mafuta ni milioni 1 kama utaenda Songea'-JPM #UzinduziNdege
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
'Tulianza na kulipa 40% na walipomaliza tulimalizia 60% na tuna mpango wa kununua ndege nyingine 2 kubwa na fedha zipo'-JPM #UzinduziNdege
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
'ATCL lilikuwa linajiendesha si kiueledi, lilikuwa limebweteka, wafanyakazi wanafanya kazi kimazoea'-JPM #UzinduziNdege
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
'Viongozi, wakurugezi wa ATCL walikuwa wanajilipa 50000 kila wanapotembelea uwanja wa JNIA wakikagua utendaji wa shirika'-JPM #UzinduziNdege
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
'Wengine ndege hizi wamenunua kwa bei kubwa lakini sisi wenye Cash tumenunua kwa bei ya chini'-JPM #UzinduziNdege
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
'Tulipochukua hatua ya kuwashika RAS, DED Kagera leo balozi wa Uingereza ametuchangia Bil 6 kwa ajili ya wananchi Kagera'-JPM #UzinduziNdege
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
'Tuna mpango wa kununua ndege zingine 2, moja itakuwa ya kubeba watu 160, nyingine itakuwa inabeba watu zaidi ya 240'- JPM #UzinduziNdege
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
'Tuliamua Serikali tununue moja kwa moja halafu tuwakodishie ATCL ili waache kufanya kazi kwa mazoea'-JPM #UzinduziNdege
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
'Niwaombe watanzania tusipuuze vitu vyetu, hata kama hutaki kwa nini usikae kimya' -JPM #UzinduziNdege
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
'Ndege hizi haZitumiki Tanzania tu, Marekani wanazo 40'-JPM #UzinduziNdege
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
'Wapo waliosema ndege hizi hazitembei ni kama bajaji, hebu fikiria imetokea Canada mpaka Dar es salaam'-JPM #UzinduziNdege
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
Ndege mpya za AirTanzania zinatarajiwa kufika kwenye viwanja 12 ikiwamo Dar, Z'bar, Dom, Mwanza, Arusha, Bukoba, Tabora, Mbya #UzinduziNdege
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
Waandishi na ninyi mnatumika kuichafua nchi yenu, kwa hiyo tutangulize uzalendo wa nchi yetu'-JPM #UzinduziNdege
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
'Natamani siku moja malaika washuke wazime mitandao yote hili baada ya mwaka wakute tumeshatengeneza TZ mpya, wanapost vingine vya ovyo-'JPM
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
'Ingekuwa ukipewa Urais miaka miwili na nusu unaachia ningefurahi kwa sababu kazi hii ni mateso hulali unafanya kwa ajili ya Watanzania'-JPM
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
'Huyo aliyesema ndege hii haikimbii awe mtu wa kwanza mimi nitamlipia nauli halafu akae mbele akaone mawingu yanavyopiga'-JPM
— millardayo (@millardayo) September 28, 2016
ULIKOSA ZIARA YA RAIS MAGUFULI KWENYE BANDARI YA DAR ES SALAAM? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI