Mwimbaji staa Alikiba amefunguka kuelekea mchezo wao baina yake na Timu ya Samatta ambapo amesema kesho ni Fainali na wao wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi wa kwenye mchezo huo ambao unachezwa Azam Complex Chamazi kwenye mechi ya hisani kwa ajili ya Watoto njiti wakishirikiana na Doris Mollel Foundation chini ya Doris Mollel.
“Tumejiandaa vizuri na mechi ya kesho, mechi ya safari hii inaushindani mkubwa Sababu ni fainali, haimanishi tunamaliza kampeni yetu namaanisha kwamba wao wameshinda mara mbili na sisi tumeshinda mara mbili, Droo moja so hii tutaona nani atamfunga mwenzake”
“Tunawashukuru wote waliojitolea kupitia kampeni hii sababu tunachokifanya hii ni kurudisha kwa Jamii na ndio maana ya Samakiba Foundation, jezi zipo na kesho zitauzwa pia uwanjani”