Kama utaweza kuwasha radio yako na kujiunga na CloudsFM kila Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa moja usiku utakutana na mtu wako wa nguvu Millard Ayo ambaye kazi yake ni kuzikusanya stori kubwa 10 za siku kutoka kwenye maisha, muziki, michezo na mengine.
#AMPLIFAYA #Aug262015 #10 Na club ya Songea Majimaji nayo imechukua kocha mpya msimu huu, ni raia wa Finland.. wamo Wachezaji wapya pia.
— millard ayo (@millardayo) August 26, 2015
#AMPLIFAYA #Aug26 #9 Majabvi wa Simba aliyecheza Vietnam anasema Nyama ya Nyoka inaliwa na Matajiri Vietnam, inauzwa ghali sio kama ya Chura
— millard ayo (@millardayo) August 26, 2015
#AMPLIFAYA #Aug26 #8 Zimamoto Mwanza wanasema chanzo cha nyumba nyingi kuungua mwezi huu ni Umeme wa TANESCO, pale unaporudi ghafla.
— millard ayo (@millardayo) August 26, 2015
#AMPLIFAYA #Aug26 #7 Mganda aliyeandamana na Nguruwe mpaka Bungeni amekutwa nje ya nyumba yake jana, hakujulikana aliko kwa zaidi ya wiki.
— millard ayo (@millardayo) August 26, 2015
#AMPLIFAYA #Aug26 #6 Watu 130 wamenyongwa Saudi Arabia toka 2015 imeanza, ni kwa hatia za mauaji, ujambazi ,ubakaji na dawa za kulevya.
— millard ayo (@millardayo) August 26, 2015
#AMPLIFAYA #Aug26 #5 Polisi Ruvuma imepiga marufuku vyama vya siasa kutumia Walinzi wao kwenye Kampeni, wanasema Polisi watalinda wenyewe.
— millard ayo (@millardayo) August 26, 2015
#AMPLIFAYA #Aug26 #4 Watanzania saba wamekamatwa Garissa Kenya wakielekea Somalia kujiunga na Al Shabaab, mmoja ni Mwanamke..
— millard ayo (@millardayo) August 26, 2015
#AMPLIFAYA #Aug26 #3 Mahakama ya Kisutu imemuachia Waziri wa zamani Lawrence Masha baada ya kukamilisha dhamana, alipelekwa Segerea jana.
— millard ayo (@millardayo) August 26, 2015
#AMPLIFAYA #Aug26 #2 James Mbatia asema leo ‘Usipotenda haki kwenye uchaguzi, Watanzania wataidai haki hiyo kwa nguvu na kwa lazima’
— millard ayo (@millardayo) August 26, 2015
#AMPLIFAYA #Aug26 #1 Mbatia >> ‘Tumezuiliwa kupatumia Jangwani kuzindua kampeni za UKAWA, Manispaa imegoma kusema nani atautumia siku hiyo’
— millard ayo (@millardayo) August 26, 2015