January 10, 2019 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ametoa siku 10 kwa Mkandarasi anayesambaza umeme wa REA katika Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma kuhakikisha amesambaza umeme katika kila Kijiji na Kitongoji na endapo atashindwa kufanya hivyo atamchukulia hatua ikiwemo kumuondoa.