Umepita mwaka mmoja tu toka msanii wa muziki wa Pop, Marekani, Ariana Grande aachie Album yake iliyopewa jina, My Everything… Good news ni kwamba msanii huyo mwenye miaka 22 amerudi tena kuziweka headlines kwenye kurasa za burudani.
Ariana Grande amerudi na single mpya kutoka kwenye Album yake mpya inayotegemea kuwa sokoni hivi karibuni, wimbo unaitwa ‘Focus’ na kizuri zaidi kuhusu ujio wa single hii ni kwamba video yake ipo hewani tayari… Single hii ni single ya kwanza itakayopatikana kwenye Album yake mpya.
Single mpya ya Ariana inapatikana kwenye iTunes kwa wale watu wangu wanaotumia huduma ya iOS na Apple Music lakini kama video mpya ya Ariana Grande haijakufikia, basi karibu uicheki video hiyo hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.