Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Arsenal Vs Aston Villa – nimekusogezea matokeo hapa

on

(null)

Wakiwa hawajafunga goli hata moja tangu December 20 – wakati Christian Benteke alipofunga goli dhidi ya Manchester United, Aston Villa leo walisafiri hadi jijini London kwenda kukipiga na Arsenal.

Mchezo huo uliomalizika hivi punde umeisha kwa Villa kucheza takribani dakika 600 bila kufunga goli hata moja – baada ya kukubali kupewa kipigo kizito zaidi msimu huu cha magoli 5-0.

Olivier Giroud alianza kuifungia Arsenal baada ya pasi nzuri ya Ozil, kabla ya mjerumani huyo nae kuongeza la pili na Theo Walcott akafunga la tatu na kuipeleka Gunners mapumziko wakiwa mbele kwa 3-0.

Kipindi cha pili Santi Cazorla akafunga la nne kwa mkwaju wa penati kabla ya Hector Bellin kufunga la tano mwishoni kabisa mwa mchezo huo.

Tupia Comments