Habari za hivi punde kutoka Sky Sports News zimedai kuwa Arsenal wametoa ahadi kwa West Ham na kuwaambia ni lini wanapaswa kutarajia makaratasi ya mikataba kufanyika leo ijumaa .
Arsenal wamewaambia klabu hiyo kwamba makaratasi yatasainiwa na kuwasilishwa hii leo na walitoa ahadi hii baada ya West Ham kuonekana kuchanganyikiwa kuhusu ucheleweshaji huo.
Mkataba huu umekuwa ukiendelea kwa wiki kadhaa na kila mtu, pamoja na mashabiki wa Arsenal, watataka dili hili likamilishwe haraka iwezekanavyo.
Rice ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu na bila shaka anastahili kuchezea klabu inayoshindania mataji.