FIFA ilisema inatoa tiketi 20,000 za bure kwa michezo ya Kombe la Dunia la Wanawake huko Auckland, Hamilton, Wellington na Dunedin huku kukiwa na wasiwasi juu ya kasi ndogo ya mauzo huko New Zealand.
Wenyeji mwenza Australia wamechukua sehemu kubwa ya tiketi milioni 1 zilizouzwa hadi sasa, na timu yake ya ‘Matildas’ ikionekana kuwa tishio la ubingwa.
Afisa Mkuu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Sarai Bareman amesema ni vigumu zaidi kuwavutia mashabiki kwenye viwanja vya soka nchini New Zealand kutokana na kiwango cha chini cha mchezo huo nchini humo, huku timu ya ‘Football Ferns’ ikiwa bado haijashinda mechi katika mechi tano zilizopita za Dunia.
Mshirika rasmi wa tukio la maonyesho la mwaka huu, Xero, atatoa tiketi 5,000 za ziada kwa michezo katika miji minne mwenyeji wa New Zealand.