Askari wa Jeshi la Polisi aliyekuwa anafanya kazi katika kituo cha Polisi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani namba E 6472 Yusuph Said (52), amekutwa amejinyonga hadi kufariki dunia katika nyumba yake anayoijenga maeno ya miembe saba Kata ya Kongowe Wilayani Kibaha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Januari 18 majira ya saa 12 jioni.
Kamanda Wankyo amesema Yusuph alikua akitumikia katika kituo C anaishi Picha ya ndege lakini siku ya tukio alienda Kongowe eneo ambalo anaendelea na ujenzi na ndipo alipokutwa amejinyonga na kamba.
Kamanda Nyigesa, amebainisha kuwa, uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea wakati taratibu za kumsafirisha marehemu kuelekea mkoani Lindi kwa maziko zikiendelea.