Hii inatokea mara nyingi kwa wasanii wengi duniani kuacha kuimba nyimbo ambazo zimewatoa kipindi wanaanza muziki,tunawaona wengi sana ukihudhuria baadhi ya show zao unakuta nyimbo wanazoimba ni zile ambazo zimefuata baada ya ile iliyowatoa.
Miongoni mwao husema wanaangalia mazingira ya wimbo huo wakati anautoa ulikua unagusa umri gani na watu gani,kutoka Mkubwa na Wanawe Aslay ambaye zamani alikua anatumia jina la Dogo Aslay amezungumzia hili>>’Dah unajua hata mie najisikia vibaya sana napouimba wimbo huu jukwaani’
‘Inanibidi tu kuimba maana ndiyo wimbo ulionitambulisha mimi kama mimi kuna sehemu nimeshawahi kufanya show bila kuperfoam wimbo huu kama Mwanza na Zanzibar na watu wananielewa nadhani Yamoto imesaidia lakini pamoja na hayo huwa natembea nayo’
‘Mimi kwa sasa nishakua mtu mzima kumwambia mtu naenda kusema kwa mama dah sema ndo vile maana ndo imenifanya mimi kuwa hivi,kwa sasa sehemu nikiombwa na mashabiki kuimba inabidi niwaimbie’.