Diwani wa Kisarawe 2, Issa Zahoro amemuomba Rais John Magufuli aendelee kukusanya vyanzo muhimu vya mapato kutoka katika Halmashauri na kuviingiza katika Serikali Kuu.
Akizungumza katika mkutano wa Madiwani, Zahoro amesema kama halmashauri hazijatafuta njia za kujiongezea mapato zenyewe hadi kutegemea Serikali Kuu basi kuna uwezekano zikaja kuvunjwa.
“Mheshimiwa alipochukua mapato kwa miaka mitatu naona kuna reflection kubwa, tuna maeneo makubwa ya ardhi ukiiuliza halmashauri inafanyia nini hakuna majibu, namuunga mkono na azidi kutafuta vyanzo vingine, tulikuwa tunakusanya mapato ya leseni za biashara kwa miaka iliyopita nini kimefanyika ?,”
Pia Diwani Zahoro amesema kama haitoshi, ikiwezekana Rais apunguze hata posho za madiwani na vikao vipungue ili ziingie Serikali Kuu kwa ajili ya maendeleo.