Kama utakuwa unakumbuka mnamo July 16, 2016 Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) lilitoa rasmi tamko la kuufungia wimbo wa msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego PALE KATI kutokuwa wa kimadili.
Sasa leo July 27, 2016 millardayo.com imepata taarifa nyingine iliyotolewa na BASATA kuhusu kumfungia msanii huyo kwa muda usiojulikana kutokana na makosa matatu.
‘Ni kweli kwamba tumetoa tamko hilo tulifuata sheria na kanuni labda nizungumzie kile ambacho kilichotufanya tuchukue maamuzi hayo, moja nadhani mnakumbuka ilikuwa tarehe 16 mwezi wa saba Baraza la Sanaa ilitoa taarifa kwa umma kuhusu kuufungia wimbo wa Msanii huyo Pale Kati kutokana na maudhui ya mule ndani’- Godfrey Mngereza
‘Kwahiyo hivi karibuni tulikaa tena kikao na akakiri kwamba kweli wimbo wake haupo kimaadili pia tukaona ngoja tumfungie kwa muda usiojulikana kutokana na tamko la wizara kuhusu maadili ya wimbo huo, alitoa wimbo wa Pale Kati na kuusambaza bila Baraza la Sanaa kuwa na taarifa yoyote kwahiyo ndio maana tukaona ngoja tumpe adhabu’- Godfrey Mngereza
ULIIKOSA HII YA BASATA KUHUSU KUUFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO ‘PALE KATI’ BASI BONYEZA PLAY HAPA KUMSIKILIZA GODFREY MNGEREZA AKIELEZEA SABABU HIZO