Mjadala wa matamshi ya Mbunge wa Kenya Charles Kanyi maaarufu kama Jaguar kuhusu kuwapiga na kuwafukuza Raia wa kigeni wanaofanya biashara Kenya wakiwemo Watanzania, Waganda na Wachina bado upo kwenye headlines ambapo Mastaa mbalimbali wa Tanzania wamesimama kupaza sauti zao.
Msanii AY ameandika yafuatayo “JaguarKenya Mimi nawajua Watanzania wenzangu kuliko wewe tumia haya maneno haya muhimu kuwaambia Wananchi hii issue iishe tuendelee na mambo mengine.. sema hivi- SAMAHANI…NIMEKOSA…NIMEKOMA … NA SITARUDIA TENA -Ni mimi mshkaji wako Ambwene Allen Yessayah (A.Y)”
.