Klabu ya Azam FC imekamilisha nafasi zake saba za kusajili raia wa kigeni kufuatia sheria iliyowekwa na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) ambalo linaruhusu kusajili wachezaji wasiozidi saba raia wa kigeni.
Usajili huo unakuwa pigo kwa golikipa Nelson Lukong raia wa Cameroon na Ryan Burge raia wa Uingereza ambao wote walikuja kufanya majaribio na Azam FC.
Azam FC imetangaza kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya Allan Wanga aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Al Merrikh ya Sudan.. Allan Wanga amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Klabu ya Azam FC.
Stori za mwanzo ilikuwa Allan Wanga na Nelson Lukong Bongaman golikipa kutokea Cameroon aliyekuwa anakipiga katika klabu ya AS Vita Club ya Congo kushindwa kufikia makubaliano na Azam FC baada ya kugoma kufanya majaribio ili kocha Stewart Hall aangalie viwango vyao kabla ya kuwasajili.
Kufuatia usajili wa Allan Wanga Azam FC imemaliza nafasi zote saba za kuwasaji wachezaji wa kigeni, hadi sasa Azama FC imewasajili Serge Pascal Wawa, Kipre Tchetche, Kipre Michael Balou kutokea Ivory Coast na Jean Baptiste Mugiraneza kutokea APR ya Rwanda, Didier Kavumbagu kutoka Burundi, Brian Majwega kutokea Uganda na Allan Wanga aliyekamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni.
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.