Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo Jumapili ya December 20 kwa michezo mitatu kupigwa. Dar Es Salaam katika uwanja wa Karume JKT Ruvu walikuwa wenyeji wa Coastal Union wakati Mbeya City walikuwa wenyeji wa Mgambo JKT. Wakati uwanja wa Maji Maji Songea, Azam FC walikuwa wageni wa Maji Maji FC.
Mchezo kati ya Maji Maji FC dhidi ya Azam FC ndio mchezo uliokuwa unatajwa kuwa na mvuto kutokana na timu za Dar Es Salaam huwa zinashindwa kupata matokeo chanya katika viwanja vya mikoani. Hata hivyo mchezo huo ulitawaliwa na mvua, lakini hiyo haikuizuia Azam FC kuondoka na point tatu.
Azam FC walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya wenyeji wao Maji Maji FC, timu ya Azam FC ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli la kuongoza dakika ya 11 kupitia kwa mshambuliaji wao wa kimataifa wa Burundi anayekipiga katika klabu hiyo Didier Kavumbagu na Ame Ally 19, wakati Maji Maji FC walipata goli la kufutia machozi kupitia kwa Alex Kondo dakika ya 54.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Tanzania bara December 20
- JKT Ruvu 2 – 2 Coastal Union
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.