Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Baada ya Kim na Kanye – Ronaldo na mpenzi wake nao wala shavu

on

Bn_QOpaCEAAStDrJarida la Vogue la Marekani mwezi uliopita liliwatoa kwenye cover wapenzi wanaotarajiwa kufunga ndoa hivi karibuni Kim Kardashian na Kanye West, na mauzo ya jarida hilo yakawavunja rekodi ya cover za nyuma za jarida hilo, baada ya mafanikio hayo inaonekana Vogue sasa wamenogewa.

Jarida la Vogue lakini safari hii la Hispania limeamua kujibu mapigo ya wenzao wa US kwa kuwaweka kwenye cover mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo na mchumba wake mwanamitindo Irina Shayk.

Irina ambaye ni raia wa Urusi ni mmoja wa wanamitindo maarufu duniani, kwa pamoja na Ronaldo, Vogue wanategemea kuuza nakala nyingi sana la jarida lao hilo linalotarajiwa kutoka mwishoni mwa mwezi huu.

Kama unataka stori kama hizi zisikupite ungana na mimi kwenye twitter kwa kubonyeza HAPA, pia FACEBOOK & INSTA ili niwe nakutumia kila stori inayonifikia.

 

Tupia Comments