Imeripotiwa kuwa Baba mzazi wa mwanamuziki Rihanna, Mzee Ronald Fenty mwenye umri wa miaka 66 amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail umeeleza kuwa mzee huyo anaendelea na matibabu katika hospital iliyopo karibu na nyumbani kwake mjini Babados.
Hata hivyo Mzee Fenty amesema anaendelea vizuri kiafya na mwanae Rihanna amekuwa akiwasiliana naye mara kwa mara kujua maendeleo yake ya kiafya.
“Nilifikiri Nitafariki kiukweli ila naendelea vizuri, Rihana amekuwa akifuatilia maendeleo yangu kila siku” – Ronald Fenty ( Baba Rihana)