Mshambuliaji wa kimataifa wa Italia Mario Balotelli ambaye huwa ni kawaida kuwa katika headlines mbalimbali kutokana na tabia yake na matukio yake ambayo anafanya, August 27 kaongea sababu zilizomfanya asifanye vizuri akiwa Liverpool.
Balotelli alikuwa na maisha magumu Liverpool kwani msimu uliomalizika aliishia kucheza mechi 16 na kufunga goli moja pekee. Balotelli analaumi mbinu za kocha wa Liverpool Brendan Rodgers ndio zimemfanya ashindwe kufanya vizuri msimu uliopita.
“Lazima nikubali makosa yangu, mfumo uliyokuwa umechaguliwa na Rodgers haukuendana na mimi, wakati naanza nilikosa nafasi kadhaa za wazi, nilikuwa na nafasi chache za kufunga kwa bahati mbaya ukichanganya na majeruhi, sikulalamika niliheshimu maamuzi ya mwalimu na nilijiheshimu kama mchezaji professional”>>> Balotelli
“Tabia zangu sio tu kwa sababu nimekuja Milan hata wakati nipo Liverpool mfumo wa maisha yangu na tabia zangu zilikuwa kawaida, kwa mfano mwaka uliopita sikuwa na tatizo lolote katika maisha yangu binafsi zaidi ya kupiga picha nikiwa kwenye migahawa na kuweka Instagram lakini hiyo haikuwa na maana kuwa sikuwa nikifanya mazoezi lakini sikucheza”>>> Balotelli
“Nimeambiwa nibadilike nifuate mfumo wa Milan nitafanya hivyo bila tatizo lolote, nimekuwa na staili hii ya nywele kwa muda mrefu ila sitaendelea nayo tena, matatizo yangu hayakuwa ubora wangu ila tabia nimekuwa nikiambiwa maneno mengi sana”>>> Balotelli
Mario Balotelli amerudi AC Milan ya Italia ikiwa ni baada ya kuondoka msimu uliopita na kujiunga na Liverpool kwa ada ya uhamisho ya pound milioni 16 amerudi AC Milan akitokea Liverpool kwa mkopo wa muda mrefu.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos