Michezo

FullTIME: Hat-trick ya Suarez yaipelekea Barcelona hii furaha..

on

May 14 2016 kuliendelea michezo kadhaa katika ligi ya Spain Laliga ambapo michezo miwili yakuamua nani atakuwa mshindi wa kombe hilo kwa msimu wa 2015/2016 ilichezwa masaa sawa, Granada walikuwa wenyeji wa Barcelona wakati wapinzani wao Real Madrid walikuwa wakikipiga na klabu ya Deportive La Coruna.

Mchezo wa Granada Vs Barecelona ulimalizika kwa Barcelona kuibuka na ushindi wa jumla ya magoli 3-0 magoli ambayo yalifungwa Luiz Suarez katika dakika ya  22, 38, 86 ya mchezo na kuifanya Barcelona kuibuka na ushindi kwenye Mchezo huo.

Mchezo wa pili ulikuwa kati ya Deportive La Coruna dhidi ya Real Madrid ambapo Real Madrid walifainikiwa kuondoka na ushidhi wa Magoli 2-0 magoli yaliyofungwa na Cristian Ronaldo katika dakika ya 7, 25 ya mchezo.

Baada ya kumalizika michezo ya leo Barcelona wametangazwa kuwa mabingwa wapya wa msimu 2015/2016 katika Ligi ya Spain (La liga)

Video ya Magoli ya  Granada Vs Barecelona

https://www.youtube.com/watch?v=8vDBf-Ico38

Video ya Magoli ya Deportive La Coruna VS Real Madrid

https://www.youtube.com/watch?v=8xwEP27MIq4

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE 

Soma na hizi

Tupia Comments