Ingawa haijatoka rasmi taarifa za upatikanaji wa madini ya dhahabu kutoka Samunge Loliondo ila inasemekana vijana wengi kwa sasa wameamua kwenda kujaribu bahati yao kwenye madini hayo amabyo yanasemekana kupatikana huko.
Taarifa kutoka kijijini mpaka sasa zinasema kuwa watu wanaongezeka kijijini hapo kwa ajili ya kujipatia madini hayo ambayo mahali yanakopatikana ni katika mashamba ya watu na maeneo ya kingo za mto katika Kijiji cha Mgongo kilichopo jirani na kwa Babu.
Baada ya taarifa hizi millardayo.com imeenda hadi makao makuu ya Wizara hiyo kwa ajili ya kujua undani wa taarifa hizi,Badra Masoud ambaye ni Mkuu wa mawasiliano kwa umma kutoka Wizara ya Nishati na madini ameanza kwa kusema>’taarifa hizo hata sisi tumezikia’
‘Taarifa hizi zinafanyiwa kazi kwakweli madini yanawezekana pale yapo ila sasa hatuwezi kuacha haya mambo yaende tu sisi tunapitia kwenye taasisi zetu,kwa mfano pale madini watu wanasema yapo kuna Shirika letu la GST ambalo lenyewe ndiyo linashughulika moja kwa moja na kuangalia masuala ya madini kama kweli yapo au hayapo’
‘kwa hiyo bado tunalifanyia kazi suala hili,kingine tuna makamishna wetu maeneo mbalimbali yakiwemo huko huko Arusha,Kilimanjaro nk. na wenyewe kule lazima wafuate taratibu na wanachohimiza ni kuwa kama wewe umeona kweli kuna sehemu ina madini lazima uombe leseni’.