Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Karim Benzema amezidi kuingia katika headlines baada ya zile stori za kuvuja kwa kanda ya ngono kuendelea kuchukua nafasi, Jumatano ya November 4 Benzema aliripotiwa kukamatwa kwa kosa hilo ila leo November 5 amefikishwa mahakamani.
Staa huyo wa Real Madrid aliyekuwa akihusishwa kuhamia katika klabu ya Arsenal ya Uingereza katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August 2015 ameingia katika kashfa hiyo pamoja na rafiki yake wa utotoni ambaye anacheza naye katika timu ya taifa ya Ufaransa Mathieu Valbuena.
Mshambuliaji huyo inatajwa katozwa faini sambamba na kufungiwa kuonana na mchezaji mwenzake wa ufaransa, hata hivyo ripoti ya kichunguzi kutoka Ufaransa zinasema kosa alilolifanya Benzema lingeweza kumfanya afungwe jela miaka mitano ila taarifa kutoka kwa mwanasheria wa staa huyo Sylvain Cormier ameviambia vyombo vya habari kuwa mteja wake hana hatia.
Benzema aliyekuwa anasumbuliwa na majeruhi na Mathieu Valbuena waliachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa mapema mwezi huu. Benzema kwa sasa anatoka na Analicia Chaves ambaye alikuwa mpenzi wa staa wa soka wa Ubelgiji Axel Witsel lakini aliwahi kuhusishwa kutoka na msanii wa pop kutoka Marekani Rihanna.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.