Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Skendo ya kutaka picha za utupu yamtafuna mpiga picha wa Kim Kardashian

on

Inaelezwa kuwa mpiga picha wa zamani wa mwanadada Kim Kardashian, Marcus Hyde ameingia matatizoni hii ni kwa mujibu wa mtandao wa TMZ ambao umeripoti kuwa mpiga picha huyo amekuwa akitaka picha za utupu kwa wanamitindo ili kufanya nao kazi.

Inaripotiwa kuwa Marcus Hyde aliwahi kufanya mawasialiano na mwanamtindo mmoja na kumuahidi kufanya nae kazi (Photoshoot) kwa zaidi ya shilingi milioni 4 za Kitanzania au atamfanyia kazi hiyo bure endapo atatuma picha zake za utupu ili amuangalie kama atafaa kufanya nae kazi.

Mpiga picha huyo ambaye aliwahi kufanya kazi na mastaa mbalimbali akiwemo Kim Mardashian,Ariana Grande ,Jhene Aiko, Childish Gambino wameibuka na kupiga vita vitendo hivyo anavyofanya Marcus Hyde hata hivyo Kim mmefunguka na kusema hakuwahi kupata shida akiwa anafanya nae kazi na anasikitishwa kusikia malalamiko kutoka kwa wanamitindo hao.

“Nimekua nikisoma meseji zote pamoja na stori kutoka kwa wanawake ambao wanafanyiwa tabia ambayo siyo nzuri kutoka kwa mpiga mpicha ambaye niliwahi kufanya nae kazi. Kutokana na uzoefu wangu siku zote na taaluma yangu nimesikitishwa na kuhuzunishwa kuona wanamwake wengine wanapitia kitu cha tofauti”

“Nasimama kwa ushirikiano mkubwa na kila mwanamke kutopitia manyanyaso, kudhulumiwa au kuombwa kitu kwa ulazima bila kuwa na amani nacho hatuwezi kuruhusu tabia kama hii iendelee na nitawapa hongera wale wote watakaoongea kuhusu hili” >>> aliandika Kim Kardashian kupitia Insta story yake.

VIDEO: CHEKI SHILOLE NA USAFIRI WAKE MPYA WA BAISKELI

Soma na hizi

Tupia Comments